Letter to the future sentinels of Humanity

Paul Jourdy (1805-1856) - Homer Reciting His Verses, 1834 ® RMN-Grand Palais /Dist. Foto SCALA, Florence


Barua kwa walinzi wa siku zijazo wa Binadamu

Solomeo, 30 Disemba 2022

Katika hizi siku zinazokaribia mwisho wa mwaka, watu wengi, kwa utulivu wa mioyo yao, wanatazama matukio yaliyopita na kuchunguza historia yetu ya hivi karibuni na ya zamani; katika kipindi hichi cha mapumziko tunatazama upeo wa siku zijazo, mawazo yangu yanawafikiria ninyi, vijana. Ninawapenda sana, na ninawaangalia kama baba yenu na mtu ambaye daima hufikiria kwa roho yake maisha ya siku zijazo. Kwangu mimi ninyi ni kama chumvi ya dunia, mmeshakuwa watu wazima na nyie ndio walinzi wa kesho, wenye kustahili, kama binadamu wengine, kuishi kwa raha na furaha. Macho yenu yanang'aa na yamejaa nguvu nyingi: sikuzote mimi huona kwamba maisha yako yanaweza kuwa yenye furaha, matumaini mazuri, na pia wakati mwingine yenye masikitiko. Ni jambo la muhimu sana macho yako yaking'aa, wakati mwingine ninapojikuta katika hali ya kibiashara, huwa naachana na hali ya kawaida na kufuata hali isiyo ya kawaida, na nazungumza nawe kwa njia rahisi kama ninavyoongea na ndugu. Nilipokuwa na umri kama wako, sikutofautiana sana na wewe. Leo mimi ni mtu aliyetimiza ndoto yangu maalamu, na nilifanikiwa kutimiza lengo nililoliwaza tokea zamani, nilizaliwa na baba yangu mzazi aliyekuwa na machozi na hasira akiwa kazini, kwa sababu alikuwa anataka kutimiza ndoto yake ili yeye na wenzake wawe na maisha mazuri kama binadamu.

Mara nyingi mimi hufikiri kwamba hicho ndicho kimefanya lengo langu liwe la maana. Kwa hiyo, wakati mwingine, tunapokuwa pamoja katika hafla fulani ya umma, macho yangu yakiwa yamekutana na yako, bila kupepesuka, huwa napenda kusimulia maisha yangu, na jinsi ninavyotambua leo kuwa umaskini wangu wa utotoni ulikuwa kama zawadi na sio hukumu, ingawa nilikuwa maskini sikukosa chochote, chakula kilikuwepo, na haswa furaha, na furaha hii, ndiyo ilikuwa utajiri wa kweli, nilikuwa na furaha kila siku ya kuishi katika mazingira mazuri ya asili: mapambazuko meupe kama yungiyungi, anga ikiwaka buluu na nyekundu, jua likichomoza na kukausha polepole umande, sauti ya mvua inayonyesha msituni, mabadiliko mazuri ya majira.

Mara nyingi mimi nawaambia kwamba utajiri sio rahisi kupatikana, si raisi kuubeba, na kama utaweza kuigeuza ikawa zawadi ndipo utapokubalika kama wewe ni mtu mwenye haki. Ikiwa kawa bahati mbaya, mkawa na huzuni maishani, yaani ile huzuni inatakayokuja siku za mbele, kama adui anayesubiri na kujificha ili awavamie kila mmoja wenu. Lakini wakati huo huo maumivu, kama vile wasomi wengi wa kale walivyotufundisha, ni zawadi, na kama Oscar Wilde alivyosema, akiwa kifungoni kwa zaidi ya miaka miwili katika gereza la Reading, "maumivu ni zawadi bora kuliko vitu vyote vilivyoumbwa."

Ninasema nawe, nikihamasishwa na ujana wako, kuhusu manufaa ya kuona ulimwengu kwa njia inayofaa. Usipoweza kutazama mbali, hutapata sababu nyingi za kuishi maisha halisi. Lakini kuona mbali ni jambo muhimu ya kila maisha yenye furaha endelevu, na ni kati ya zawadi zenye thamani zaidi ambazo tumepokea kutoka kwa wanadamu. Leon Battista Alberti, aliyechora jicho lenye mabawa liwe alama ya nembo yake, alilijua vizuri. Macho yanafanywa kuangalia mbali, mbali iwezekanavyo, kuangalia upeo wa macho, kama Alexander Mkuu alipokuwa bado mtoto, alikuwa akiishi masaa mengi ukingoni wa pwani na macho yake yalikuwa yanatizama mwisho wa bahari, na moyo wake ulikuwa kwenye mstari wa bluu unaotenganisha anga na maji, alifikiria nchi hizo ambazo alikuwa anataka kuziteka ili kuunganisha tamaduni kubwa zaidi za ulimwengu katika kipindi hicho. Ukiweza kuangalia mbali, vijana wapendwa, mtakuwa na uwezo wa kufikiria na kugeuza ndoto ili muwe na maisha mazuri, na utatambua alama za nyakati, ambazo hazina haraka wakati ukitaka kufikia malengo makubwa, ya wakati huo ambayo yanaonekana kuwa ni madogo ukilinganishwa na mwaka au mwangaza, lakini inaanza kwenda upesi ukilinganishwa na karne moja au zaidi. Ili uweze kutimiza ndoto yako, angalia anga. Penda sanaa, penda uzuri, kwa kuwa ndani yake kuna ukweli unaounganisha nafsi na ulimwengu halisi. Epuka ghadhabu, ambayo huvuruga njia za roho na kuzuia mbingu kukupa baraka zake.

Mpaka sasa, sisi kama wazazi tumefanya makosa mengi yaliyotufanya tuwaze kuwa kufanya kazi ni adhabu ya kutokuwa na akili shuleni, na wakati mwingine matumaini yanafifia. Sasa ni wakati wa kuanza maono mapya: si rahisi kumiliki nafsi yako, lakini wewe ni miongoni mwa wale wanaoweza kufanya hivyo. Halafu, unapotamanishwa na mvuto mzuri wa maua au na harufu ya matunda yaliyoiva ambayo nyuki huyafuata, wakati upepo, ukivuma kwa kupenda kwake, unaonekana kwako kama Mercurio unaotangaza nchi za mbali, na kupita kwake ni muziki mzuri sana, basi utakuwa katika hali ya furaha ya tumaini na ya ulimwengu wenye mgaro unaokusubiri.

Soma vitabu: kama Mfalme Hadrian alivyodhania, kujenga maktaba ni kama kujenga maghala ya umma. Sio lazima kujifunza kila kitu; ikiwa kitabu ni kitabu kizuri, kilichoandikwa na wale ambao wameishi na roho ya kibinadamu na kusema ukweli kwa maneno rahisi, au ambayo yana hekima ya watu wa kale, ukisome kwa nasibu, kila asubuhi katika ujana wako mzuri na kisha katika maisha yako mazuri, na usisome zaidi ya mistari kumi na mbili ya vitabu utakavyokuwa unasoma. Ni njia ya kufurahisha na yenye faida ya kuanzia siku, na usisahau kwamba pamoja na akili inayotokana na elimu sikuzote kuna akili ya nafsi yako.

Kamwe usiogope kufanya makosa, kila mtu anafanya makosa, na ni kwa sababu ya kufanya makosa ndio tunaweza kujirekebisha tena; usione aibu kulia, kwa sababu, kama dereva mkubwa wa mbio Ayrton Senna alivyosema, machozi ni mafuta ya roho. Kumbuka kwamba tendo moja zuri huondoa makosa mengi. Usihisi kamwe kwamba wewe ni bora zaidi kuliko wengine, kwa sababu nafsi zetu huwa zina nafasi ya mawazo mazuri. Uwe unawafikiria watu wengine, katika upendo wako wa familia, katika masomo yako, katika kazi yako, katika maisha yako ya mapenzi, kwa sababu ikiwa utaendelea kujifikiria sana mwenyewe, njia sahihi haitapatikana kwa uhakika. Ili tuwe na furaha sana sio lazima tuwe na kitu tunachopenda, bali tupende kitu kinachostahili kupendwa.

Eeh Muumbaji utulinde!

Brunello Cucinelli

Close
Select your language