
Solomeo (Italia), Novemba 2020
Nilizaliwa kijijjini kwenye familia ya wastani, na huko, usiku nyota zilikuwa zina mwanga mkali, unahisi kuwa Kiumbe kimekamilika; tulihisi ulimwengu uko ndani ya maisha yetu , tuliona kwa undani kanuni kuu za ushirikiano wake. Katika maisha yangu nilikuwa nataka kuweka maadili na heshima kwa adhama ya binadamu katika kanuni za juu zaidi, na kutokana na matarajio haya nimejaribu kujishughulisha na biashara ya kuuza Cashmere, na kuzalisha kwa uangalifu zaidi bila kuharibu Viumbe, kuendeleza uwiano wa kudumu kati ya faida na urejeshaji.
Nikiwa na shauku kuhusu falsafa, niliweza kuthibitisha, nikisoma Kierkegaard, kwamba hatima ya binadamu na ya ulimwengu zimeingiliana, na hii ina thamani kubwa kwangu. Nimekuwa nikiamini ubinadamu kama kipengele cha ulimwengu; haya yalikuwa mawazo makuu ya watu wa zamani, kuanzia Dante hadi Galileo; kila mmoja kwa njia yake mwenyewe, alichanganya ubinadamu na mambo ya kiroho na sayansi. Nasema kwamba mtu hawezi kuishi bila ubinadamu, na nimeamua iwe ndiye rafiki mwaminifu wa roho yangu: na kutokana na hayo nimefikiria wazo langu la ubepari wa kibinadamu, na kisha, kufikiria anga zenye nyota wakati wa utoto wangu, wazo la hatima ya binadamu na ulimwengu.
Haswa kwa sababu ya kupendezeshwa na maisha ya ujana wangu, kwa sababu ya mtazamo usio na kikomo, navifikiria Viumbe kama mlezi anayejali ambavyo tunafaa kushukuru kwa zawadi nono tunazozipokea kwa ukarimu mwingi; Ninaishukuru sana kwa Viumbe hivi. Lakini kwa muda sasa, mwaka huu, maisha yetu yamezungukwa na msafiri ambaye hakutarajiwa wala kuhitajika, ambaye kwa njia ya janga la virusi anazunguka sayari nzima anasababisha maumivu ya kimwili na kiroho kwa binadamu, kwa zoezi isiyotabirika na inayochosha, wakati mwingine polepole, wakati mwingine kwa haraka, wakati mwingine kwa upole, wakati mwingine kwa ukatili, na matumaini yanayobadilika na kutegemewa na baadaye kukatisha tamaa upesi.
Inaonekana tunashuhudia mvutano fulani kati ya bayolojia na dunia, ambayo yanadumu kwa muda mrefu, na hapa, hatimaye, Viumbe vyenyewe umetuomba sisi msaada. Sasa naamini ni juu yetu sisi, binadamu, kwa wajibu wa kimaadili, kuitikia wito huu muhimu na wenye haraka; na ninafikiria aina fulani ya mkataba mpya wa kijamii na Viumbe.
Mkataba wa kijamii ni wazo la zamani, tokea enzi za Plato, Aristotle, na baadaye, hivi karibuni, Thomas Hobbes na John Locke, na mwishowe Rousseau, aliyeandika kitabu kuhusu hilo suala. Mkataba ninaoufikiria ni mpya kwa sababu sio tu unawahusu binadamu, lakini inahusu kila kipengele kingine cha Viumbe. Milima ya mbali, misitu minene yenye giza, bahari kubwa na zilizochafuka, anga za bluu zenye nyota chini yake kuna wanyama na mimea yanayoishi kwa uwiano wa kudumu, ninawaona, pamoja na binadamu, ambaye ni dhamana muhimu ya mkataba mpya, na ninawawakilisha, kama ulimwengu wote, kama paraiso ya kidunia ya nyakati zetu, ulimwengu uliokuwa umevutia na matakatifu bila mipaka, Iliyosambaa sehemu zote zilizo mbali kwenye kona zote zana Viumbe.
Labda, hata hivyo, hivi karibuni tumepuuzia kwa kiasi fulani sheria kadhaa za asili ambazo kwa muda mrefu zimekuwa ndio misingi ya aina halisi na ya ukweli ya maisha; labda tumepoteza uwiano uliokuwa unapokea na kurejesha kwa usawa katika uhusiano uliopo kati yetu na Viumbe, na tumeanza kuuteketeza, badala ya kuutumia kulingana na mahitaji ya asili na yenye umuhimu, kama alivyohubiri Epicurus pamoja na mamia ya vizazi visivyo na majina waliohubiri kabla yetu.
Kwa hiyo, tukiangalia katika mioyo yetu na ujasiri wa ukweli, kama, kulingana na mawazo ya Kant, kwa macho yetu tunaangalia mbingu iliyopo juu na kuhoji sheria za maadili ndani yetu, tutatambua hilo tumekuwa watoto wapotevu, na kisha, kama ilivyo wakati kuungama hadharani tukiwa wengi kwa pamoja, tutatambua kwamba kama Viumbe ukitaka msaada wetu leo, sisi pia tunawajibika kwa mateso yake.
Kwa hiyo tuwafikirie watoto wetu, vizazi vijavyo, ambao kuliko kitu chochote kingine ndio tumaini la kesho; hebu tufikirie ulimwengu watakaorithi kutoka kwetu, ambao unapaswa kuwa mzuri kiasi kuliko huu; hebu tufikirie urithi wa zamani, ambazo bila hizo, kama wanafalsafa wanavyofundisha, hakuna siku za baadaye. Kama tukisahau mafundisho ya zamani, tunawezaje kufuata njia salama ya kimaadili? Inaonekana kwangu kuwa tuna deni kwa vijana ambao sisi tumewachukulia muda wao, matumaini yanayofuata maadili; na macho yao yatayatafuta macho yetu, ambayo huwa yanakwepa, kwa sababu sio rahisi sisi kujibu kwa sura kakamavu na za kweli kama zao.
Na pia inafikiria kwa hofu ya upendo ya vizazi vijavyo ambayo ninawaza kuwa mkataba mpya wa kijamii na Viumbe, kwa sababu ningependa watoto wa binadamu wa leo wawe na uwezo wa kuishi katika sayari ambayo wanyama, mimea, na maji, wanapata muda na sehemu, ya kujitengeneza upya kulingana na mazingira, na midundo mipana na yenye utulivu ambayo yameashiria wakati wa historia ya binadamu katika milenia; wakati na mahali ambapo misitu hurudi tena kuichukua duniani, kuiondoa kutoka kwenye jangwa, kuirejeshea dunia oksijeni na hewa baridi.
Kwa hiyo napenda kuota ndoto kuwa vizazi vijavyo vitaweza kuishi sehemu wanazotaka watatambua nchi yao, na kwenye dunia nzima watafanya wanachotaka; wataona uhamiaji mkubwa wa watu kama fursa na sio hatari, ikiwa watazingatia kurekebisha na kutumia tena vitu na kuendeleza desturi hiyo na sio kuharibu, kama Serikali na sheria hazitaonekana kama majukumu ya kulazimisha ila ni maisha ya kistaarabu ya kuheshimika kama maisha yenye haki; kama wakijua jinsi ya kuendeleza teknologia na ubinadamu kama madada wanaopendeka, kama sehemu zote za dunia zitazingatiwa kama torati ya kila mmoja wetu na mwishoni, kama, jinsi alivyowaza Mfalme Hadrian wanajua jinsi ya kuzingatia vitabu kama ghala za nafsi, watakuwa na furaha. Huu ndio mkataba wa kijamii ningependa kuusaini na Viumbe, huu ndio msaada ningependa kutoa kama jibu lenye upendo kwa mlezi anayenijali sana. Asante sana, na Viumbe vikaangaze njia yetu.