A tribute to the people of Mongolia and China
Kuwaenzi watu wa Mongolia na Wachina

Mara kwa mara nimekuwa nikiushukuru Ulimwengu kwa mchango wake katika maendeleo ya viumbe vyake vyote; leo hii, baada ya kipindi cha huzuni duniani kote, ninajisikia kama mtu aliyepata mrejeo wa furaha na matumaini moyoni, kwani napenda zaidi kufikiria jinsi gani hili janga limeweza kuninufaisha na sio kufikiri jinsi lilivyoweza kuniathiri. Nikiwa kama Marco Polo mpya, natoa shukrani zangu kwa watu wawili ingawa wako mbali bado nahisi wako karibu nasi. Kimwili wako mbali lakini kiroho wako karibu.

Ni kwa sababu ya watu hawa wa Mongolia na Wachina kwa ujumla ambao ni wenye majivuno, waungwana, watu wa kale na wenye utu wa kibinadamu, wanaofanya kazi kwa bidii na wenye sifa za kujinyima, wabunifu, wakarimu na wako wazi kwa ulimwengu, na pia kwa nyuzi zao za Cashmere zenye ubora wa hali ya juu, nimefanikiwa kutengeneza kwa miaka kadhaa, na kwa njia ya kiufundi na umahiri wetu hapa Italia, na kutupatia bidhaa bora, na ajira kwa watu wengi. Ni kwamba nyuzi zao za joto zilizo laini, ziko kama za kimungu, zimeniwezesha kutimiza ndoto yangu ya kibepari na ya kibinadamu, ambapo maelewano kati ya faida na zawadi kutoka kwa Mungu ni kipaumbele cha juu zaidi, na pia watu wote ni ndugu na juhudi kubwa zinafanywa ili maisha yao yawe ya kirafiki zaidi, miji yao iwe ya amani na utulivu, vitongoji vyao viwe vizuri kuishi na mashamba yao yawe na rutuba. Ninapenda kile ambacho Confucius aliwahi kusema: «Mtu mwenye ukarimu, anayetaka kujiendeleza mwenyewe, hupenda pia kuwaendeleza wengine». Huwa ninafikiri kuhusu ukuaji wa kiroho, na sio tu kuhusu ufanisi wa vitu vya kimwili.

Hawa watu wa Mongolia na Wachina, ingawa wako mbali lakini pia wako karibu kiroho wamenikaribisha mara nyingi sana wakati wa safari zangu za kibiashara: nitawezaje kusahau anga yao isiyo na mipaka na nyasi zao zenye majani ambayo upana wake mkubwa unanikumbusha jinsi Ulimwengu ulivyo mkubwa na vifananisho vya kibinadamu katika familia? Hapa, nimefurahishwa na utu wa kibinadamu na nimejionea mwenyewe walivyo na subira pamoja na huruma, na ninaweza kusema kwa moyo wote kwamba nilifurahishwa sana na wema wao, na walivyonikaribisha, au tuseme, wamefanya nijione kama mimi ni mtu. Ilikuwa usiku wenye nyota kali, chini ya mbalamwezi inayoangaza mwanga wake kwenye nyasi na milima inayozunguka inayoweza kuonwa kufikia upeo wa macho na kwamba nilivutiwa na uzuri huo na nilianza kuwaza nchi yangu ya asili, iliyo mbali sana, ingawa mandhari yake yanafana. Ilinikumbusha mandhari yaliyokuwa karibu na mji wa Castelluccio, uliokuwa karibu na Norcia, katika eneo nilalolipenda la Umbria, panafanana kidogo na Mongolia, kwa kuwa ina mikunjo ileile ya ardhi na kuna eneo kubwa la kijani, na pia kuna mchanganyiko ule ule wa rangi za anga wakati wa machweo. Na pia nilifikiria kuhusu upendo wa mazingira, yaani ukweli uliopo kati ya uhusiano wa binadamu na Ulimwengu - ambapo binadamu anaishi, pamoja na vitu vyote vilivyo Ulimwenguni - na kuhusu kuheshimu wanyama, hata kama wanaliwa kama chakula; wakati wanapochinjwa, wanaona kuna haja ya kuwaomba wanyama msamaha na kuwaeleza kuwa dhabihu yao ni muhimu na ina ulazima; na ndivyo maneno ya Epicurus yaliponiijia akilini mwangu. Na nikajiuliza: Je! Kuna njia bora zaidi ya kukaa vizuri na kuishi Ulimwenguni? Je! Kuna njia, sehemu, au kipindi ambacho hisia zetu na mtazamo wetu wa Ulimwengu una maana zaidi, yaana ukweli, na yanatuhusu moja kwa moja!? Watu hawa, ambao sitawasahau kamwe, walinifanya nielewe, kwa njia rahisi na ya kawaida, kwamba inawezekana. Hili ndilo wazo nililokuwa ninawaza, na kufikiria, yaani kuwepo na mkataba mpya wa kijamii na Ulimwengu, yaani makubaliano mapya yasiwe tu na binadamu, bali yawe pia na ardhi, maji na wanyama; kuenezi Ulimwengu, mlezi wetu mkubwa, ambaye amempa binadamu faida nyingi, ila sasa anaonekana kama anahitaji msaada wetu, na sisi tunaona, kama vile ni jambo la kawaida, na kwamba hatuhitaji kumpa jibu.

Na nimerudi tena kwenye ubinadamu wangu wa Kiitaliano, kwa jinsi ninavyoichukulia katika mwelekeo wa kiulimwengu zaidi, na ghafla nimeelewa, nimefumbua macho yangu na nimeona wazi ufahamu wa kina na wa kuelimisha neno kuu linalomhusisha mtu: "ndugu". Ninajua ni maarifa gani na utamaduni wa kiasi gani ambao hawa watu wameupa ulimwengu wa Magharibi na Mashariki kwa milenia iliyopita. Na, kusema ukweli, ni lazima nitaangalia leo historia iliyopita, ambayo ni ndefu na ilichangia mengi, na kama ni kumtafuta mtu ambaye, kati ya watu kadhaa, ndiye mwakilishi mkuu wa historia ya Wachina, falsafa na roho, atakuwa Confucius; ndiyo maana, katika nyumba yangu iliyopo kijijini kwetu Solomeo, nimemuezi mtu huyu katika mahali pa heshima mwongoni wa watu wenye busara waliokuwa wanaishi enzi hizo; picha yake, iliyochongwa kwenye jiwe, inakaa karibu na ile ya mtu mwingine mwenye hekima, mwanafalsafa wa kale wa Uigiriki ambaye alikuwa anaishi wakati wa Confucius: Plato. Kile kinachowafananisha ni ujuzi mkubwa ambao wameuletea ulimwengu, ujuzi ambao umedumu kwa muda mrefu sana.

Nilipokuwa, katika safari zangu za kibiashara, nikiwa kama mgeni niliyekaribishwa mezani kula chakula na hawa watu, niligundua roho ya kiulimwengu iliyopo ndani ya kila mmoja wao, na ndani ya nafsi yao niliona mafundisho ya mwanafalsafa wangu mpendwa na mkubwa Confucius, ambaye alisema «ninasambaza lakini siumbi».

Ninawaangalia hawa watu kwa mtizamo wa mtu wa Magharibi, ninaangalia macho yao mazuri ya rohoni, ambayo yanaonekana yamepakwa wanja kiufundi, yenye siri nyingi na ufadhili, na ninaona uwazi na ukweli wao, nia yao ya kutaka kukujua, kukushirikisha na mambo yao, mawazo na hisia zao. Unachohitaji kufanya ni kuangalia mifumo yao ya uandishi, ambayo ni sanaa ya kipekee - kila neno ni kama picha iliyochorwa - au kuishi karibu na hawa watu mashuhuri kwa muda kidogo ili kuelewa kitu ambacho vinginevyo huwezi kuelewa, k.m. jinsi umbali na ukaribu unavyoweza kuishi kwa pamoja na uhusiano uliopo kati ya kanuni hizi mbili; kuna jambo ambalo linatuunganisha na watu hawa: familia.

Dante, kwa hekima zake, alinifundisha kuwa kila chaguo tunalofanya ni tendo la upendo na kwamba nyuma ya matendo yetu yote kuna matukio yetu ya zamani, fundisho lenye umuhimu mkubwa kwangu, na ni kwa sababu hiyo nimeamua kuwashukuru milele, kutoka chini ya moyo wangu hadi kina ya roho yangu, watu wa Mongolia na Wachina kwa nyuzi laini na za thamani za cashmere ambazo ni kiashirio cha uzuri wa Ulimwengu, kwa ujumla, na hiyo kwangu, inaashiria ushirika wa binadamu.

Close
Select your language